February 5, 2020

MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa mchezo wake wa jana Februari,4 mbele ya Simba ulikuwa ni mzuri walichoshindwa ni uzoefu tu kupata pointi tatu mbele ya Simba.

Polisi Tanzania ilikubali kufungwa mabao 2-1 mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Hamsini amesema kuwa wachezaji walionyesha uwezo wao wote na walijitahidi kupambana mbele ya wapinzani wao.

"Nawapa pongezi wachezaji wangu wameonyesha kile ambacho niliwaambia wafanye na walijitahidi kwa kweli. Kilichotushinda ni uzoefu tu kwani bado timu inajijenga taratibu na kuendelea kutafuta matokeo mazuri," amesema.

Polisi Tanzania imecheza jumla ya mechi 19 imefikisha pointi 30 ipo nafasi ya saba kwenye msimamo.

Kwenye mchezo huo walianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Sisxtus Sabilo aliyekuwa msumbufu mwanzo mwisho dakika ya 22 na yale ya Simba yakifungwa na John Bocco dakika ya 56 na Ibrahim Ajibu dakika ya 90.

12 COMMENTS:

  1. Huyo kocha muungwana kweli mwenye kuijuwa kazi yake Bila kuyatamka yale maporojo wanayotatamka wa matopeni. Hao jamaa wajitazame vizuri kwasababu Balinye waliyemtimua kageuka nyota huko Kenya Katika mchezo wake wa Kwanza

    ReplyDelete
  2. Aaah kumbe unajua kuna goli la off side ndo maana unamsifu kocha wa polisi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakuna goli la offside ...ni wimbo wa vyura vya matopeni..wameanzisha propaganda ambazo zitarudi kuwaumiza wao. mwaka jana wimbo ulikuwa viporo viporo.hivi Yanga wangecheza viporo vyao namna Simba ilivyocheza wangekuwa hapo walipo...kila timu ifanye mambo yao..,wao watembee juu ya mpira...Simba wao wanatembea juu ya point tatu

      Delete
    2. nadhani wewe kutoa comments hapa ni makossa sana vile mpira huujui tokana na kuikataa offside ya wazi ambayo hata wachambuzi baada ya mechi waliafiki kua ni offside . comments ziwe zinajenga mpira na sio za ushabiki usio na dhima

      Delete
    3. hakuna goli la offside pale ni propaganda za vyura!Na Yanga wawe na kumbukumbu wakati wa Malinzi na Mwesigwa walikuw hata ubingwa wanapewa buree

      Delete
  3. Kutokana na malalamiko Yao ya uongo yasiyokwisha ndio mana ndio mana wamekuwa wakitolewa maanani. Hao jamaa wangecharuka Namna gani ingelikua lile goli alilofunga Amisi Tambwe goli ambalo Kwanza aliunawa kwa mkononi na kushuhudiwa na kila mtu na kukubaliwa na Reda, je Ingekuwa goli kama lile kwa njia ikele imefungwa Yanga, wangekaa kimya kama ilivofanya Simba iliyistaarabika? Simba iliamuwa kupuyza na kunyanaza kimya

    ReplyDelete
    Replies
    1. aliestaarabika alivunja viti au umesahau !!!!

      Delete
  4. Shabiki ndio waliovunja viti na sio simba.

    ReplyDelete
  5. Mimi ni refarii na ninasema haikuwa offside.Mabeki wa Polisi walijichanganya na kuivunja offside wenyewe.kilichowafanya wale mabeki wawili kurudi kumkaba Bocco nini?Jibu ni kuwa walirudi kumzuia/kumbugudhi Bocco asifunge goli.Walipaswaa kumpotezea Bocco kama vile hawana habari naye.Msiwahukumu marefarii Kwa mihemko na kutafasiri Sheria 17 za soka wakati hata Sheria no 1 hamjui inasemaje.Tumesomea urefarii na hatufuati kile mnachokitaka.Angalieni video clip ya hilo goli na sio picha mgando.Kwa nini mabeki walirudi kumkaba Bocco na akafunga mbele yao?Mabeki waliivunja offside wenyewe.Kucheza offside trick inahitaji akili ya ziada na game plan against timu pinzani unayocheza nayo.Simba formation ni kuua offside trick na ndio maana wanatumia viungo wao Kwa kupiga pasi mpenyezo ambazo mabeki pinzani wakijisahau na kufungwa wanakimbilia Kwa linsmen kulalamika ni offside.Angalizo kwenu wachezaji kuwa msitegemee sana maumuzi ya marefarii na hii iliwa cost sana hiyo Simba kwenye klabu bingwa ya Africa walipokuwa wanafungwa goli 5 kwani walikuwa wanafunguka sana mchezoni na kujisahau na kukuta wanafungwa magoli waliodai ni offside.Jitafakarini kabla ya kututolea shutuma ambazo mtoa tafsiri wa Sheria hizi 17 ukimpa filimbi apulize itajaa mimate tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tupe jina lako kama kweli wewe ni referee maana maelezo yako yana utata na tukiwa na mareferee wenye mtazamo wako itakua ni shida katika mchezo wa mpira wa miguu nchini mwetu maana huwezi kutudanganya watu ambao Maisha yetu yote tumecheza na tunaangalia mipira ya kila kona duniani na tunazijua sheria vizuri

      Delete
    2. Kuwa umecheza mpira na kuangalia mpira kila Kona ya dunia haijalishi kuwa unazifahamu vyema sheria 17 za mpira.Ikiwa marefarii waliobobea ktk kazi yao pale kwenye ligi EPL wanashindwa kutafasiri goli la halali au hapana kiasi kuletewa VAR ni vipi umtolee povu refarii wa VPL(T) shutuma za kuwa wanahongwa,wanawabeba timu fulani?kwangu lile goli siwezi kulaumu maumuzi ya kuwa ilikuwa sio goli halali sababu sijui kama ilikuwa offside kwani hakuna aid device(VAR) ya kutuamulia na hivyo uamuzi wa refarii ni wa mwisho na Sheria ndivyo inavyosema.

      Delete
  6. Hujui sheria wewe labda ukafunue sasaivi usome,ila kaa ukijua hata simba ilifungwa magoli matano kwa mfumo wa aina hii ndugu zangu,makocha hawa wanatumia akili sana na endapo marefa wanakua ni wababaishaji hapo kila kukicha simba angehesabia maumivu ila kiuhalisia hakuna holi la off side,na hiyo dhana itaathiri klabu pinzani mtajikuta mnaathirika kisaokolojia,ambapo matokeo yake hayatakua mazuri hivyo ningeshauri epukeni hiyo dhana ikiwezekana ifutwe kabisa,kingine lazima ujue sio kila anaecheza mpira basi anajua kwamba hii ni off side,tambua kwamba kuna off side hata marefa wa epl hawawezi kugundua ndiomana kuna VAR,hivyo dhana yako ya kwamba eti tunacheza mpira na tunajua sheria haikizi kutetea kwamba ile kweli ilikua off side.upeo wako mdogo sana ndiomana upo hapo na laiti kama ungelikua na upeo huo unaojipa nakujidhania kwamba unao basi ungelikua umekalia kiti nakupewa majukumu,japo sio wote ni watendaji,jifunze lugha ya kiungwana mbele ya jamii,TANZANIA ni nchi ya amani sana na upendo,midahalo kama hii usipende sana kusiamama upande ambao utakua kama mchochezi ambapo mwisho wa siku lazima itakuletea effects wewe mwenyewe,ni ushauri wangu kwako kutokana na mtazamo nilio nao japo sio lazima kuufuata maana neno langu si shera,sitaki povu plz.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic