JOHN Bocco
nahodha wa Simba amefunga mabao matatu ambayo yameacha gumzo ndani ya Bongo
kutokana na kufunga mabao yake kwa miguu yote miwili ya kulia na kushoto huku
akifunga kwa kutumia mguu wa mwisho ambao
amepewa pasi.
Yaani kwenye mabao yake matatu mchezaji wa mwisho akimpa pasi kwa mguu wa kulia naye anafunga kwa mguu wa kulia na akipewa kwa mguu wa kushoto anafunga pasi kwa mguu wa kushoto.
Bao la
kwanza alifunga Uwanja wa Taifa kwa mguu wa kulia kwa pasi ya Clatous Chama
aliyotengewa kwa guu la kulia dakika ya 57, ilikuwa Februari 4.
Bao lake la
pili alifunga mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri , Februari 11 alifunga dakika
ya 45 kwa guu la kushoto kwa pasi ya Meddie Kagere aliyotengewa kwa guu la
kushoto na kupachika bao lake la pili msimu huu,
Simba ilishinda kwa mabao 3-0.
Pia alitoa pasi ya kwanza kwa guu la kulia iliyoleta bao lilifungwa na Hassan Dilunga kwa
guu la kulia.
Februari 15
alipachika bao lake la tatu na la ushindi kwa Simba mbele ya Lipuli na Simba
ilishinda kwa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu Uwanja wa Samora, Iringa,
alifunga kwa guu la kushoto dakika ya 22 alipewa pasi kwa guu la kushoto na Francis
Kahata mwenye jumla ya pasi nne za mabao na amefunga pia mabao sita..
0 COMMENTS:
Post a Comment