STEVEN Bergwijn, nyota wa Spurs alifungulia balaa la mabao mbele ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliomuacha Pep Guardiola akiziacha pointi tatu zikiyeyuka jumla.
City ilichapwa mabao 2-0 kwenye mchezo huo ambapo Bergwijn alifunga dakika ya 63 kisha Son Heung-Min alipachika bao la pili na la mwisho dakika ya 71.
Mabingwa watetezi walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Oleksandar Zinchenko kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 60.
Ushindi huo unaifanya Spurs ya Jose Mourinho kuwa nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 huku City ikiwa nafasi ya pili na pointi 51 zote zimecheza mechi 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment