February 3, 2020


Hali inazidi kuwa mbaya na hatari ya utandawazi inaonekana maana leo hii mashabiki wa soka nyumbani Tanzania wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na klabu ya Aston Villa ya England bila ya kipingamizi chochote.

Mashabiki Watanzania wamekuwa wakiandika kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta wakilalamika kuwa ananyimwa pasi na Jack Grealish.

Kwanza si kweli lakini tujifunze kuwa wastaarabu maana tayari baadhi ya mashabiki wa Villa kutoka England wameanza kujibizana na wa hapa nyumbani ambao ni wageni katika klabu hiyo wakiwaita PLASTIC FANS.

Tafadharini sana, tuwe waungwana na hakuna sababu ya kumtengenezea Samatta uadui na wachezaji wenzake au mashabiki wake kwa kuwa sisi tuko mbali huku.

Hakuna mwenye ushahidi kwa Grealish kumyima pasi Samatta, huu ni ushabiki wa Kibongo ambao unajengwa na kulaumu kila jambo.

Grealish anahusika katika kupiga bao la Kwanza la Samatta EPL, anahusika kwa kumpa Samatta pasi safi ambayo alikosa bao la wazi dhidi ya Leicester City.

Grealish ndiye mchezaji anaongoza kwa kutoa pasi nyingi, kapiga 800 zilizofika, ana asisti 5, ana mabao 7. Si kweli anamyima pasi Samatta na vizuri tuwe na takwimu wakati tunalaumu. Na kama kuna tofauti kidogo, basi wanaweza kuyamaliza kwa kuwa wote ni professional players.

Hivyo vizuri tumpe nafasi Mbwana Samatta apambane badala ya kumuwekea ugumu.... CHONDE CHONDE WAUNGWANA..... Tusisikilize tu na kukubali, tutafakari kwanza.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic