February 16, 2020


Mkurugenzi wa Manchester United, Ed Woodward amesema anaona nafasi ya kikosi chao kufanya vizuri msimu ujao huku akiamini msimu huu wanaweza kutwaa mataji ya Europa na FA.

Hivi karibuni Woodward alivamiwa nyumbani kwake na kundi la mashabiki wa Manchester United waliokuwa wakishinikiza aondoke sababu amekuwa akilegalega kufanya usajili wa wachezaji ndani ya timu hiyo.

“Naona tunaelekea njia nzuri, usajili wa Bruno Fernandes na wachezaji waliopo majeruhi wanarejea taratibu kikosini, ni dalili njema kwetu, uhakika ni mkubwa kufanya vizuri msimu ujao ila msimu huu tunaweza kutwaa Kombe la Europa na FA.

“Tangu Ole Gunnar Solskjaer ameichukua timu anajua kipi cha kufanya, sisi viongozi tunamuunga mkono kwa kila kitu, usajili tuliofanya chini yake umefanikiwa kwa kiasi kikubwa tofauti na misimu iliyopita,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic