Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Watanzania hawana budi kuonesha mapenzi yaliyopitiliza kwa Mtanzania Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Aston Villa ili wasimuharibiwe kwenye Klabu yake mpya na mazoea na wachezaji wenzake.
Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, ambapo amesema tabia ya Watanzania kuacha kuandika maoni yao yasyokuwa na tija kwa hatna ya Mbwana Samatta.
'Kama unampenda Samatta na umevamia nyumba ya mtu mwingine ishi kama wanavyoishi kama wale, msianze kuleta mambo ya kutukanana, badala yake mnaanza kumgombanisha Samatta na wenzake.' amesema Waziri Mwakyembe
'Niwaombe Watanzania tupunguze mapenzi ya kupitiliza kwa Samatta bali tumuombee' ameongeza Waziri Mwakyembe
Tazama video kamili hapo chini
CHANZO: EAST AFRICA TV
CHANZO: EAST AFRICA TV
0 COMMENTS:
Post a Comment