Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakari Malima, amesema kuwa kiwango cha timu hiyo kwa sasa kimezidi kuongezeka.
Malima ameeleza namna uchezaji wa Yanga unavyoenda hivi sasa inaonesha ni namna gani timu inajengeka.
Mkongwe huyo aliyetamba miaka ya nyuma amefunguka akieleza Yanga ilikuwa inapitia wakati mgumu kwa kuangalia na uwepo wa wachezaji wengi ambao ni wapya.
Jana Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa kunako Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment