February 4, 2020


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana habari na tuzo ya mfungaji bora ila anachotazama ni rekodi mpya kwa timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

Simba imetwaa mataji 20 ya ligi ikiachwa kwa jumla ya mataji 7 na wapinzani wao Yanga wenye mataji 27, endapo watafanikiwa kulitwaa msimu huu watabakiza deni la mataji sita kufikia rekodi ya watani zao.

Msimu wake wa kwanza Bongo 2018/19, Kagere alifunga mabao 23 katika ligi na timu yake ilitwaa kombe kwa mara ya pili mfululizo ikimaliza na pointi 93, huku ikifunga mabao 77.

Kagere alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kumpa nafasi ya kufanya kile anachokipenda akiwa uwanjani jambo ambalo kwake ni furaha.

“Nafasi yangu na kazi yangu inaniruhusu kufunga na kutengeneza mabao, ninamshukuru Mungu kwa hili, mashabiki pia nawashukuru kwa kuwa wananipa sapoti ila nitazidi kupambana kufikia malengo kwani kazi bado inaendelea,” alisema Kagere

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic