February 4, 2020


MZAZI wa mshambuliaji wa Aston Villa ya nchini Uingereza, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta, amemtaka kijana wake huyo abadili mwenendo katika klabu yake hiyo mpya ili kuhakikisha anakuwa bora zaidi ya alivyokuwa KRC Genk ya Ubelgiji alikotokea.

Samatta amesajiliwa katika Klabu ya Aston Villa hivi karibuni, akitokea Genk kwa dau la pauni milioni 8.5 huku akijiwekea rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kujiunga na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Aidha nahodha huyo wa Taifa Stars tayari ameshaichezea timu yake hiyo mechi mbili, ikiwa ni dhidi ya Leicester katika nusu fainali ya Carabao Cup ndani ya dakika 65 huku akishindwa kufumania nyavu licha ya kukosa bao moja la wazi.

Pia, juzi Jumamosi, Samatta alifumga bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, pia likiwa ni bao pekee kwa Aston Villa ambao hata hivyo walishindwa kutamba ugenini mbele ya Bournemouth ambao waliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Mzee Samatta alifunguka kuwa, kama mzazi amejisikia vyema kuona mtoto wake huyo anakipiga katika ligi kubwa duniani lakini amemtaka aongeze juhudi zaidi ya alivyokuwa mwanzo.

“Nimefurahi kuona mwanangu anakuwa Mtanzania wa kwanza kuchezea ligi kubwa duniani, kwani mzazi yeyote amekuwa akipenda kuona mwanawe anafikia mafanikio.

“Kitu ambacho nimemtaka akifanye kwa sasa ni kuhakikisha anaongeza juhudi mara mbili zaidi ya ile aliyokuwa akiifanya Genk kwa kuwa ligi hiyo ni kubwa na ina ushindani zaidi, hivyo ajipange kuhakikisha anakuwa katika kiwango bora,” alisema mzee Samatta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic