Na Saleh Ally
TUMEKUWA na kawaida ya kubadilisha uchukuliaji wa mambo. Yale ya kawaida tukayapa uzito sana na mazito tukayachukulia kuwa mepesi tu, nafikiri ni utamaduni.
Kuna wakati unalazimika kubadili mambo kadhaa ili kuwa kwenye utaratibu mzuri ambao ni sahihi. Si jambo jema kufanya mambo bila ya kutafakari.
Kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humud, amefanya kitu ambacho hakikuwa sahihi na kinatengeneza makwazo kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar lakini inawezekana viongozi, makocha na hata wachezaji wenzake.
Wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita, Mtibwa Sugar walilala kwa bao 1-0 na baada ya mchezo huo, Humud ambaye ni kiungo mkongwe, alibadilishana jezi na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi.
Baada ya hapo, Humud alikwenda moja kwa moja kuhojiwa na Azam TV na alionekana akiwa na jezi hiyo. Hili si jambo baya, soka si uadui na hiyo ndiyo fair play.
Alipotoka katika mahojiano hayo, Humud alikwenda moja kwa moja hadi eneo walipo mashabiki wa Yanga na kuanza kupiga nao picha akiwa anaonekana amevaa jezi ya Yanga.
Hakuna ubishi, tunaona jambo hili ni la kawaida lakini katika maisha ya kiushindani na hasa kwa wachezaji, makocha na viongozi halileti picha nzuri.
Jaribu kuwaza, kwamba baada ya mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham mara tu baada ya kwisha, Salah anavaa jezi ya Tottenham halafu anakwenda upande walipo mashabiki wa Spurs na kuanza kupiga nao pia! Hili linawezekana kweli?
Au leo hii, mechi kati ya Aston Villa dhidi ya Arsenal, baada ya mechi Samatta abadilishane jezi na David Luiz halafu anakwenda upande walipo mashabiki wa Arsenal anaanza kupiga nao picha. Unaamini hili litakuwa sahihi? Najua unaweza ukasema hapana lakini kwa kuwa kule ni England. Mpira una misingi na miiko na lazima ifuatwe.
Humud ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, ingependeza kama atapiga picha na mashabiki wake wa Mtibwa Sugar ambao walikuwa pale uwanjani kumuunga mkono. Wakati mashabiki wako wanashindana na wale wa timu pinzani baada ya mechi, unavaa jezi ya timu pinzani na kwenda kupiga picha na wale wanaoshangilia timu pinzani.
Kuvaa jezi inawezekana, ingawa nayo si sahihi zaidi kwa mchezaji wa Azam FC kuwa anahojiwa akiwa amevaa jezi ya Simba au yule wa Simba aende kuhojiwa akiwa amevaa ya Mtibwa. Inapendeza kuwa na jezi ya timu yako ndiyo maana unaona wachezaji wengi hawabadilishani jezi pale uwanjani, wanafanya hivyo baada ya kuingia vyumbani ili kuepuka matukio kama hayo ya Humud.
Unaweza kusema mashabiki waliniita wenyewe, kama mchezaji unayejielewa unaweza kutambua kuwa si sahihi kufanya hivi kwa wakati huu. Mfano, Humud angeweza kupiga picha na mashabiki wa Yanga wakati mwingine barabarani au kwingineko lakini si siku wametoka kucheza na Yanga na papo hapo unakwenda kupiga na mashabiki wao.
Kuna watu wamekuwa na hisia kwamba, Humud anajipigia debe siku moja atue Yanga. Inawezekana lakini kwa mchezaji hahitaji vituko kusajiliwa na timu fulani. Huenda wengi wanaweza wakawa wanafananisha na lile tukio la Mrisho Ngassa kuvaa jezi ya Yanga wakati akiwa Azam FC tena akionyesha wazi alikuwa akifanya visa na baadaye kweli alisajiliwa Yanga.
Kama kweli Humud atakuwa anafanya hivyo kwa kufanya vituko hivyo ili atue Yanga, atakuwa hajitambui na anapaswa kubadilika. Yanga ya sasa watakuwa tofauti kidogo na watakachoangalia ni uwezo wa wachezaji na si wale wanaoipenda tu (kama sijakosea).
Unaona wakati wenzake wakiwa vyumbani, Humud alikuwa akipiga picha na mashabiki wa timu pinzani. Wakati wachezaji wakiingia vyumbani, walimu hupata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wao kabla ya kufanya maandalizi kidogo na kuondoka uwanjani hapo.
Humud kuendelea kupiga picha na mashabiki hata kama wangekuwa wa Mtibwa Sugar wakati wenzake wakiwa vyumbani ambao ni utaratibu sahihi, nayo ni sehemu ya utovu wa nidhamu.
Hata kama maandishi haya yatamkwaza, sitajali sana kwa kuwa mimi namuona Humud ni mchezaji mkongwe, anapaswa kuwa mfano katika mengi kuhusiana na soka na hasa suala la nidhamu na kufuata weledi wa anachokifanya ili awe mfano kwa vijana wanaochipukia.
Niliwahi kuandika kuhusiana naye aliposema maneno ya dharau kwa Didier Drogba nikimkumbusha hakuwa kiwango chake na baadaye naamini aliona.
Saleh Umetumwa na Hamida fc we!
ReplyDeleteShida Nini hapo
ReplyDeleteHamna ulichoandika zaidi ya kutengeneza Chuki tu
ReplyDeleteShida yawezekana Humud alirubunia na Yanga kucheza chini ya kiwango na baada ya mechi alikuwa akiigiza maonyesho feki ya fair play.
ReplyDeleteKwa sababu ni michezo yenu kurubuni wachezaji wa timu pinzani basi akili yako imeganda hapo hapo
DeleteWw saleh jembe mnafki sana2 huchambui mpira waongerea mambo yasio kuhusu mbna huongerei simba kubebwa na mitandoa tifutifu wa kazima badilika ww acha unafiki
ReplyDeleteMliocomment huko juu wote mnakalia kidole cha kati
ReplyDeleteWewe unpumuliwa kisogoni na kukalia dhakari za mabasha zako hadi marinda yote yametepeta
Delete