ZUBERI Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kilichoiponza timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Simba ni kushindwa kuwazuia wapinzani wake eneo la katikati ya uwanja.
Katwila alishuhudia mlinda mlango wake namba moja Shaaban Kado akiokota mipira nyavuni mara tatu kwa mabao ya John Bocco, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Hassan Dilunga.
"Tulikuwa bora na mipango yetu ilikuwa imara ila tulishindwa kuzuia eneo la katikati ya uwanja ambalo wapinzani wetu walitumia kutengeneza mipango yao," .
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na ina pointi 23.







E bana wee. Kocha katwila ungeongea angalau kajikauongo kidogo kuwa magoli ya Simba ni offside ili kuwafurahisha malalamiko FC.
ReplyDeleteHahahaa nakuunga mkono kwasababu wale jamaa waliweka mashikio Yao wazi kusikia kauli hizo ili wazidi kucharuka
ReplyDeleteKama goli alilofunga Lamine jana lilikuwa la offside kabisa maana alikuwa yeye na kipa Mtchana.
ReplyDelete🤣🤣🤣🤣
Deletehata goli la boko halikua sahihi baada ya kumsukuma beki na kuanguka kisha yeye kufunga lile goli na anaebisha arudie kuangalia tena video ile ni foul kama refer angekua anafanya wajibu wake angelikataa goli
ReplyDeleteChura ueshikwa pabaya
Delete