February 18, 2020

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa unajipanga kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa kesho, Februari, 19 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma dhidi ya Tanzania Prisons.

Mtibwa Sugar ilifungwa mchezo wake uliopita bao 1-0 na JKT Tanzania uwanja wa Gairo, bao pekee la ushindi kwa JKT Tanzania lilifungwa na Daniel Lyanga dakika ya 33 kwa mkwaju wa penalti.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru, amesema kuwa wamejipanga kupata matokeo mbele ya Prisons ili kurejea kwenye ubora.

"Hatujawa na matokeo bora ila kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Prisons mashabiki watupe sapoti," amesema.

Prisons mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic