SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kilichoibeba Simba jana, Februari 11, mbele ya Mtibwa Sugar ni kujituma kwa wachezaji wake.
Simba jana ilishinda mabao 3-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sven amesema:"Matokeo mazuri ni kitu ambacho nilikuwa nahitaji, hata wachezaji pia walikuwa wanalitambua hilo, kujituma kwao na juhudi zao ndio siri ya mafanikio yetu,".
Simba inafikisha jumla ya pointi 53 ikiwa kileleni baada ya kucheza jumla ya mechi 20.







Huyu jamaa ni kocha ila watanzania tumezoea makocha wenye vibweka kama makocha wa Yanga maneno mengi. Nasema ni kocha na miongoni mwa makocha bora kutua kwenye soka la Bongo kwa point zangu kadhaa. Na licha yakwamba Patrick Ausems ameifikisha Simba robo faianli klabu bingwa Africa lakini kamwe hawezi akavaa viatu vya huyu bwana mdogo. Licha ya kutwaa klabu bingwa Africa kama kocha msaidizi Cameruni lakini hahihitaji muda mwingi kwa wenye kujua makocha kukwambia kuwa huyu Sven ni kocha.(1) Msimamo wake katika kazi na kufanya kile anachokiamini kuwa ni sahihi bila ya kuyumba hata kama kuna watu wanaguna. Na hapa ni pale kocha alipohitaji kutaka kujua uwezo wa kila mchezaji na kupelekea kupangua kikosi karibu kila mechi. Kocha tayari alishasema hivyo awali yamwanzo tu alipoanza kuifundisha simba kuwa atahitaji kujua uwezo wa kila mchezaji na kama kocha mweledi basi alipaswa lazima afanye hivyo, ila wasiojua wanaojifanya wanajua zaidi wakaanza kumkosoa kocha kabla ya kukamilisha program yake.Mfano kocha alipanga fowadi mmoja mbele pekee ili kujua uwezo binafsi wa kila fowadi hapo napo ikawa balaa yaani hatari,kelele zikapazwa kocha aondoke hajui kupanga timu?
ReplyDelete(2) Utulivu wa kocha na kuongea ukweli juu ya wachezji wake pale wanapofanya vizuri au vibaya. Ukweli unauma ila ni ukweli pekee ndio utakaokutajirisha na kupokelewa kwa furaha na Bwana wa milele siku ya pumzi zikizima. Kocha wa Simba amekuwa mkweli ila tunajua kama watanzania tayari kocha ameshajijengea maadui.
(3)Kocha ni kijana na ana nguvu na hamasa kubwa ya kufanya kazi ili kujijengea C.V nzuri ya klabu na kwenye maisha yake ya kazi kwa hivyo huyu ni kocha wa kazi kwa Simba sio midodosho. Kocha ana sifa nyingi nzuri za kazi kwa wale wanaotaka kufanya kazi na kuona matokeo mazuri ya kazi. Mchezo wa Mtibwa na Simba utakupa picha kamili ya jinsi gani Sven alivyozungumza kwa kujiamini kuelekea mechi ngumu ya ugenini na kikosi chake kutimiza alichokisema ni dalili tosha kuwa kocha anajua anachokifanya na kinachohitajika ni kupewa muda na ushirikiano wa kutosha, yaani kocha na wachezaji waungwe mkono na wanasimba wote badala ya kubezwa.