February 11, 2020


SERGIO Aguero mshambuliaji wa Manchester City ni kinara kwa wachezaji waliotwaa tuzo ya Mchezaji Bora ndani ya England kwa mwezi.

Mwezi Januari baada ya kufunga mabao sita ilimfanya atwae tuzo hiyo na ana jumla ya mabao 16.

Hiyo inakuwa tuzo yake ya saba ya mwezi kwa mchezaji huyo mzaliwa wa Argentina.

Amewapiga bao wachezaji wengine ambao ni Steven Gerrard na Harry Kane ambao wameitwaa mara sita.

Aliwazidi Allison Becker, Abdoulaye Doucoure, Jack Grealish, Jordan Henderson, Ayoze Perez na beki wa Southampton Jack Stephens.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic