February 3, 2020


SIMBA kesho itashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo utakuwa wa 19 kwa Simba kukamilisha mzunguko wa kwanza sawa na Polisi Tanzania ambao wote wanamaliza mzunguko wa kwanza.

Mechi zao zote mbili za mwisho wameshinda ambapo Simba ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania ilishinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

Sven Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata ushindi utakaowafanya wazidi kuongeza nguvu ya kutafuta ubingwa na Malale Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa watapambana kupata ushindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic