KIKOSI cha
Simba leo kimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa
penalti 3-2 mbele ya Stand United kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa
Uwanja wa Kambarage.
Dakika
tisini zilikamilika kwa Stand United kusawazisha bao dakika ya 67 kupitia kwa
Miraj Saleh aliyesawazisha bao la Simba lililofungwa na Hassan Dilunga kwa
mkwaju wa penalti dakika ya 51.
Penalti kwa
upande wa Simba zilifungwa na Clatous Chama, Deo Kanda na Hassan Dilunga huku
Meddie Kagere na Ibrarahim Ajibu wakikosa penalti zao.
Kwa upande
wa Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza licha ya kumaliza mpira ikiwa
pungufu kufuatia mchezaji wao Mwente kuonyeshwa kadi nyekundu ilikaza.
Ilifunga
mabao mawili kupitia kwa Brown Raphael na Juma Ndaki.
Simba ina hulka ya ubingwa...Zahera kasema iko kwenye temple ya ubingwa..so wanaosema eti inabebwa...inanunua mechi!inapuliza dawa vyumbani watapata tabu..leo pale gongowazi wasingechomoka...kwa taarifa ya Gwambina ndiyo wako vizuri daraja la kwanza group B..salamu zaooo
ReplyDeleteTulishakubaliana wanaume wote kimya tusubiri vitendo,jukwaa lao waongee mpaka wakome wenyewe,simba piga kimyaaa.
ReplyDeleteI would like to suggest to Mr Sven to use the elite team if the target is to win such championships and not be used as a place to provide chances to players who were not lucky to participate in powerful league matches, otherwise the results could appear as we experienced during the last two seasons of similar tournaments
ReplyDeleteYes, should never underestimate the opponents and past mistakes should not be repeated
ReplyDeleteKama Stand wangekuwa wamenea bila ya mchezaji wao kutolewa kwa hila za pesa za simba kwa refa,basi leo tungekuwa tunaongea mengine maana simba alishakuwa urojo
ReplyDelete