February 25, 2020



JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa hakutarajia kama wangeweza kushinda mbele ya West Ham United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield.
Liverpool kwenye mchezo huo ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1 jambo lililomfanya Klopp akate tamaa ya kuendeleza rekodi yake ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa msimu huu wa 2019/20.
Georginio Wijnaldum wa Liverpool alianza kufunga bao la kwanza dakika ya tisa lilisawazishwa na Issa Diop wa Westham United dakika ya 12 na dakika ya 54 walifunga bao la kuongoza kupitia kwa Pablo Fornals.
Liverpool ilipindua meza kibabe kupitia kwa Mohamed Salah dakika ya 68 na lile la ushindi lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 81 na kuifanya Liverpool icheze mchezo wake wa 27 bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu England ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 79 huku West Ham United ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 24.
Klopp amesema kuwa hakutarajia kama vijana wake wangefanya maajabu makubwa na kuwataka waongeze zaidi juhudi ili kuendelea kupata ushindi kwenye mechi zao zinazofuata.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic