February 2, 2020


UONGOZI wa Klabu ya Simba umeendelea kumng’ang’ania kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili kutaka kuthibitisha kauli yake ya kudaiwa kutaka kuhongwa gari aina ya IST.

Kabwili katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini, alieleza kuwa kuna kiongozi mmoja wa Simba alimtaka afanye kosa ili apewe kadi ya njano na kukosa mchezo wa watani wa jadi kisha apewe gari aina ya Toyota IST, jambo lililozua sintofahamu.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe alisema wanamtaka kipa huyo athibitishe kauli yake aliyoitoa juu ya shutuma katika klabu hiyo huku akidai kuwa, jambo hilo siyo mara ya kwanza kwa Yanga kutoa shutuma kwa Simba na kufikisha taarifa Bodi ya Ligi na TFF.

“Simba bado tunasisitiza Kabwili athibitishe kauli yake, tulilifikisha jambo hili Takukuru ambao tumewaandikia barua pamoja na TFF na Bodi ya Ligi waweze kufanyia kazi jambo hili.

“Hii siyo mara ya kwanza kutokea kwetu, msemaji wa Yanga aliwahi kutoa maneno ambayo si sahihi na tuliwaandikia barua Bodi ya Ligi na TFF kushitaki lakini ikawa kimya, hivyo tumeandika tena kwani jambo hili siyo dogo linalenga kuzichafua taasisi hizo kuwa hazisimamii vyema mpira wa nchi hii,” alisema Kashembe.

2 COMMENTS:

  1. Ni lazima alete ushahidi. Huu ujinga wa kuharibia timu jina ni lazima ukome. .

    ReplyDelete
  2. Nilishangazwa sana Kwa nini viongozi wetu wa Simba hawakuchukua hatua ya kuwashtaki wale waliotoa shutuma kuwa Simba ilikuwa inapulizia madawa vyumba vya timu pinzani.Hii nayo iliichafua brandy ya Simba na majuzi shutuma hizi zimeendelea kusikika.Viongozi wetu wa Simba chukueni hatua ili uzushi wa kupulizia madawa vyumbani,mara tunahonga marefarii ukome.Wafikishwe kwenye vyombo husika ili wathibitishe na tuhuma wanazotoa Kwa kutoa ushahidi ili kuilinda brandy ya Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic