WAKATI uongozi wa Yanga ukiwa katika harakati za kutaka kubadilisha mfumo wa uendashwaji wa klabu hiyo, kutoka wa sasa na kwenda kwenye ule ya kibiashara zaidi, sasa mambo ni moto.
Baada ya juzi Jumamosi uongozi huo kumshusha nchini mtaalam kwa ajili ya kuja kusimamia mchakato huo wa mabadiliko kutoka nchini Ureno ambaye ni Carraca Antonio Domingoz Pinto, Mzungu huyo amewataka wana Yanga kutokuwa na wasiwasi huku akiwahakikishia mambo mazuri yanakuja.
Pinto ambaye pia amewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa vigogo wa Ureno, Benfica, amesema kuwa Yanga wategemee mambo mazuri kutoka kwake katika kipindi chote atakachokuwa hapa nchini.
Alisema atahakikisha kuwa anaifanya kazi yake ipasavyo kwa kipindi chote atakachokuwa Yanga ili kuhakikisha mchakato wa mabadiliko uliomleta katika klabu hiyo, unafanikiwa na kuifanya Yanga kuwa moja kati ya timu za kuigwa hapa nchini na Afrika kwa ujumla.
“Nashukuru Mungu nimefika salama hapa nchini na nimefurahi sana kufika salama.
“Ninachoweza kuwaambia Wanayanga ambacho wanategemea kukipata kutoka kwangu ni kwamba wategemee kupata mambo mengi ambayo yataifanya klabu yao kuwa moja kati ya klabu kubwa Afrika.
“Nitahakikisha nafanya kazi iliyonileta kwa umakini mkubwa na ni matumaini yangu kila kitu kitakuwa sawa na kuifanya iweze kujiendesha kibiashara katika soka la kimataifa,” alisema Pinto.
Katika hatua nyingine, Pinto anatarajiwa kukutana na uongozi wa klabu hiyo leo na kufanya kikao maalam kabla ya kuanza kuifanya kazi yake iliyomleta klabuni hapo.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ameliambia gazeti hili: “Kesho (jana) atakutana na uongozi katika kikao maalumu baada ya hapo ndipo itajulikana ni lini ataanza kuifanya kazi
0 COMMENTS:
Post a Comment