February 22, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuelekea Machi 8 hautakuwa na maneno mengi zaidi ya kuwataka mashabiki wakutane uwanjani kuongea kwa vitendo.

Machi 8 kutakuwa na pambano la watani wa jadi litakalowakutanisha Yanga na Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Simba inakumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye pambano la kwanza lililopigwa Januari 4 Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:-"Tunaziba kabisa mdomo kuhusu hiyo Machi nane, hapana kikubwa zaidi ya kusema tukutane uwanjani,".

4 COMMENTS:

  1. Wakianguka watani Katika mechi hiyo na kushinda mechi mbili zijazo ikiwa si 100% basi 99.9% ubingwa ni wa Mnyama. Tusubiri tuone

    ReplyDelete
  2. Wenye kupayuka wapayuke sisi tuseme kwa vitendo .

    ReplyDelete
  3. Mmeanza lini kunyamaza? Hata hayo nliyoyasema mtakaa kimya ni maneno; au hamjui?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic