February 1, 2020


THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga hawana presha nao kwa kuwa wamejipanga kuwachapa mapema ili kuzibeba pointi tatu muhimu.

Mtibwa Sugar, jana, Januari,30 ilikuwa Uwanja wa Uhuru ikimenyana na Azam FC, itarejea tena uwanjani, Jumapili, kumenyana na Yanga iliyo chini ya Mbelgiji Lucy Eymael.

Kifaru alisema kuwa wana kazi ngumu ndani ya Bongo ila mawazo yao makubwa ni kushinda mbele ya Yanga mapema ili kupunguza kelele za mjini.

“Unajua timu yetu inatoka kijijini sasa ikishinda kwa hizi timu za mjini inapendeza sana na kuzima zile kelele, tumejipanga na tunatambua kwamba mapema tutashinda na kusepa na pointi tatu.

“Yanga wanaitambua vema Mtibwa, ninaamini wanatambua kwamba watacheza na Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, tuliwafunga Visiwani Zanzibar na kuwarejesha mjini mapema watataka kulipa kisasi kwa hilo wasahau, tunazijua mbinu zao tutawapa tabu,” alisema Kifaru.

2 COMMENTS:

  1. Ujumbe kwa viongozi wangu wa Simba. YANGA kwa kupitia sport pesa na viongozi wa Yanga waliiwesesha Namungo kwa kila hali kuhahakisha Simba inadondosha points. Nadhani sio dhambi hata kidogo Simba kuiwezesha Mtibwa shuga kushinda mechi yake zidi ya Yanga ubaya ubaya.

    ReplyDelete
  2. nafikili uongozi wa simba ujipange kuaachana na sport pesa na kutafuta mzamini mwengine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic