LEO Uwanja wa Taifa kutakuwa na kazi moja tu Yanga ya Luc Eymael itamemyana na Mtibwa Sugar ya mzawa Zuber Katwila ambaye ni bingwa wa Kombe la Mapinduzi na ana kumbukumbu ya kunyoosha Yanga kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 3-2.
Rekodi zinonyesha kwamba tangu msimu wa 2011/12 mpaka 2018/19 timu hizi zikiwa zimekutana uwanjani mara 14 Yanga imeshinda mechi sita, Mtibwa imeshinda mechi nne na zimetoka sare mechi nne.
Jumla ya mabao 27 yamepatikana ambapo Yanga imefunga jumla ya mabao 15 huku Mtibwa Sugar ikifunga jumla ya mabao 12 na hakuna mshambuliaji aliyesepa na mpira.
Mechi ya mwisho iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri, Yanga ilikuwa chini ya Mwinyi Zahera na alishuhudia timu yake ikichapwa bao 1-0 hivyo leo itakuwa ni vita ya kisasi mbele ya Mbelgiji Eymael ambaye alishinda mechi yake iliyopita mbele ya Singida United kwa mabao 3-1 huku Mtibwa Sugar ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC Uwanja wa Uhuru.
Matokeo yao yapo namna hii:-2011-12 Mtibwa 0-0 Yanga,
Yanga 3-1 Mtibwa. 2012-13,Mtibwa 3-0 Yanga, Jamhuri.
Yanga 1-1 Mtibwa, Taifa. 2013/14, Yanga 2-0 Mtibwa, Taifa, Mtibwa 0-0 Yanga, Jamhuri. 2014/15, Mtibwa 2-0 Yanga, Yanga 2-0 Mtibwa.
Yanga 3-1 Mtibwa. 2012-13,Mtibwa 3-0 Yanga, Jamhuri.
Yanga 1-1 Mtibwa, Taifa. 2013/14, Yanga 2-0 Mtibwa, Taifa, Mtibwa 0-0 Yanga, Jamhuri. 2014/15, Mtibwa 2-0 Yanga, Yanga 2-0 Mtibwa.
2015/16, Mtibwa 0-2 Yanga, Jamhuri, Yanga 1-0 Mtibwa, 2016-17, Yanga 3-1 Mtibwa Sugar, Taifa.
Mtibwa 0-0 Yanga, Jamhuri, 2017/18, Yanga 0-0 Mtibwa,Uhuru, Mtibwa 1-0 Yanga, Jamhuri. 2018/19, Yanga 2-1 Mtibwa, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment