February 5, 2020


JACK Grealish, mchezaji nyota wa timu ya Aston Villa amewekwa kwenye rada za Manchester United pamoja na Leicester City ambao wanahitaji kuipata saini yake.
Nyota huyo ambaye anakipiga timu moja na Mbwana Samatta, raia wa Tanzania amekuwa akifuatiliwa kwa ukaribu na klabu nyingi kutokana na ubora wake akiwa ndani ya Uwanja.
Ameisaidia timu yake kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Carabao Cup msimu huu na amehusika kwenye jumla ya mabao tisa na kutoa jumla ya pasi tano za mabao.
Rekodi za Grealish zimezivutia timu nyingi ambazo zimeanza kumvutia kasi ili kupata huduma ya nyota huyo kwenye timu zao ikiwa ni pamoja na Tottenham .
Nyota huyo mwenye miaka 24 amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu hiyo iliyo chini ya Dean Smith ikiwa inahaha kubaki ndani ya Ligi Kuu England, ipo nafasi ya 17 imecheza mechi 25 na ina pointi 25.

1 COMMENTS:

  1. aende tu.....amwachie ufalme samata kwani nyota yake(samata) huwa inang'ara kwa staili hiyo.nakumbuka mputu alipoondoka mazembe ndipo nyota yake ikaanza kuwaka,hata alipokuwa genk kuna staa ambae alimkuta lakini alipoondoka kwenda ulaya nyota yake ikaanza kuwaka pia......hivyo naamini hata hapo alipo(Avsf),grealish akiondoka ndio utakuwa mwanzo wa kuwaka kwa nyota yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic