February 6, 2020


NAHODHA wa timu ya Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa walipewa mbinu na Kocha Mkuu Luc Eymael za kuwabana Lipuli jambo lililowapa ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Tshimbi amesema kuwa Eymael aliwaambia kwamba wanacheza na timu bora ni lazima wapambane kupata matokeo mapema jambo lililowapa nguvu ya kujiamini.

"Kocha alituambia kwamba tunacheza na timu bora na ngumu ni lazima tupambane kupata matokeo mapema jambo ambalo lilitupa matokeo haraka.

"Kipindi cha pili tulizidiwa mbinu ila tulilinda matokeo na tumefurahi kuondoka na pointi tatu muhimu,".

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi  34 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 17.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Mapinduzi Balama na Cernard Morrison wote walimaliza pasi za Juma Abdul huku lilel la Lipuli likifungwa na David Mwasa.

4 COMMENTS:

  1. hamna ushindi pale..kweli magoli ya Yanga ni halali...lakini pia kuna goli la timu timu ya Lipuli dhuruma imetokea..Katika timu zilizoishaingia kutoa rushwa Africa Yanga ni mojawapo 1983!Turudi na kwenye mchezo wa Tanzania Prison...offside na penalty tata..Nani anabebwa?Basi iwe ikitokea Yanga tunamwachia Mungu ..na ni makosa ya kibinadamu ya marefa

    ReplyDelete
  2. Goli limetokea kwenye mwamba wa goli???Lipuli wamenyimwa goli hapo .Marefa wanazingua. Ikitokea kwa Simba wanabebwa. Ikitokea kwa timu zingine makosa ya kibinadamu??Kwani kuna makosa ya kijini?Lilipokataliwa goli la Kagere wachambuzi wakasema ni kosa la kibinadamu!!!
    Akifanya kosa kwenye mechi ya Simba sio binadamu bali shetani anayeibeba Simba.
    Waandishi wacheni double standard.

    ReplyDelete
  3. halafu waandishi wote waliokuwa wanaandikwa siba inabebwa wako kimya kuhusu goli la lipuli lililodhurumiwa

    ReplyDelete
  4. Hawawezi kuandika chochote maana wameshuhudia kwa macho yao timu yao ikibebwa,amakweli yanga timu ya serikali.a.k.a ya wananchi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic