February 24, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kuambulia sare kwenye mechi zake nyingi ni ujanja wa timu pinzani ndani ya Uwanja.

Yanga imeambulia sare nne mfululizo ilianza mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1, Tanzania Prisons 0-0, Polisi Tanzania 1-1 na jana 0-0 mbele ya Coastal Union.

Eymael amesema kuwa :" Wachezaji wa timu pinzani wamekuwa ni mafundi wa kujiangusha na kupoteza muda bure jambo ambalo linapunguza kasi ya washambuliaji na wachezaji kupata matokeo,'.

Yanga imekusanya pointi 41 ipo nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 22.

4 COMMENTS:

  1. Ameishiwa sababu zisizo na uzito wala mana. Empty soun ding words.Tumtake radhi Zahera na arejeshwe kikosini kabla ya kughariki jahazi na kukimbiwa na kila mtu

    ReplyDelete
  2. Ina maana mpira unachezwa dakika ngapi, na hawa wapinzani hulala kwa takriban dakika ngapi. Yaani kocha mzima unashindwa kutoa sababu za kiufundi angalau basi sema wapinzani wanakamia na kubutua butuuu hivyo mipango huvurugika.

    ReplyDelete
  3. Kipindi cha pili mechi nä Coastal niliomba mechi iishe kwani Yanga tulizidiwa sana.Badala ya kuleta sababu za kiufundi analeta porojo. Enough is enough.

    ReplyDelete
  4. basi Luc akaziambie timu pinzani zicheze anavyotaka yeye..Akacheze basi na Azam hapo iwe Azam imetangulia ndio atamjua Razak ni nani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic