March 27, 2020

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji pamoja na mashabiki kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona kwani afya ni utajiri kwa kila mmoja.

Morrison ni ingizo jipya alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo akitokea nchini Ghana na ameanza kukubalika kwa mashabiki kutokana na kucheka na nyavu na kutimiza majukumu yake uwanjani kwenye mchezo wake dhidi ya Simba alifunga bao la ushindi.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa ajili ya kupambana na Virusi vya Corona, Morrison anapiga mazoezi nyumbani ili kuwa fiti.

"Ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhai kuhusu Virusi vya Corona kwani ni hatari iwapo wengi watapuuzia na kingine kinachotakiwa ni kila mmoja kutumia wakati huu kujilinda na kuchukua tahadhari kwa afya yake.

"Ninachukua pia tahadhari na kuwashauri wengine wafanye hivyo ili kuwa salama na kikubwa ni afya na wao kubaki salama," amesema.

Morrison amefunga mabao matatu kwenye ligi na ametoa pasi tatu za mabao wakati Yanga ikiwa imefunga mabao 31 kwenye ligi ipo nafasi ya tatu na poini 51. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic