March 27, 2020


LIVERPOOL timu inayoongoza Ligi Kuu England kwa sasa ikiwa imecheza mechi 29 na kujikusanyia pointi 82 kibindoni ipo kwenye hatihati ya kumkosa mshambuliaji wao Mohamed Salah raia wa Misri kwa muda wa miezi minne ya msimu ujao.

Hali hiyo inakuja kutokana na kuvurugika kwa ratiba za michuano mingi ya kimataifa kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Corona ambapo michuano mingi ya kimataifa imebadili ratiba zao ikiwa ni pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp tayari ameanza kupasua Kichwa kutambua ni nani atakayekuwa mbadala wa nyota huyo iwapo mambo yatakuwa kama ambavyo hajatarajia.

Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) inatarajiwa kufanyika Januari na Februari 2021 jambo litakalomkosesha pia nyota wake mwingine raia wa Senegal Sadio Mane ambaye ni nahodha wa kikosi hicho.

Kocha wa timu ya Taifa ya Misri Chini ya miaka 23, Shawky Gharib amesema kuwa mchezaji Salah ana uwezo wa kipekee na kila kocha ambaye anafanya naye kazi ni lazima ampe nafasi ndani ya kikosi chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic