UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa watendaji wao Jaffary Idd Maganga 'mbunifu' na kocha msaidizi Idd Nassor Cheche ambao wamechimbishwa ndani ya kikosi hicho wamedumu na kikosi hicho kwa muda wa miaka 10.
Azam FC kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba na wamedumu kwa miaka 10 wakiwa viongozi ndani ya Azam FC ambapo jana, Machi 2 walipewa mkono wa kwa heri.
Jaffary Idd Maganga
Alianza kazi akiwa ni Ofisa Habari wa Mbagala Market 2008
akajiunga Azam FC akianza kwenye nafasi ya mpiga picha za video wa timu kwa ajili ya kuweka YouTube.
Idd Nassoro Cheche
Mchezaji wa zamani wa Sigara ya Dar Es Salaam, yuko na Azam FC tangu inaanza. Yeye ndiye aliyempokea Salum Abubakary 'sure boy' wakati akijiunga na klabu hiyo 2007.
Yeye ni mmoja watu waliotoa mchango mkubwa katika kuifikisha hapa ilipo, akiipa mataji mawili Azam FC; ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2017 na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu 2018/2019 akishirikiana na Meja Abdul Mingange.
Cheche pia ameshiriki mafanikio ya timu ya vijana ya timu hiyo (Azam FC U-20), iliyobeba mataji manne, matatu ya Uhai Cup 2008, 2009 na 2012, pamoja na taji la michuano ya vijana ya Rollingstone mwaka 2014.
Hapo sawa hawo ndio walikuwa wanawaharibia timu yenu
ReplyDeleteKivipi?
Delete