LEO Uwanja wa Taifa, majira ya saa 11:00 jioni kutakuwa na mchezo unaosubiriwa kwa hamu kati ya Yanga na Simba ambao ni wa mzunguko wa pili ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kila timu inaamini wachezaji wake kutokana na uwezo wao wa kufanya maajabu ndani ya Uwanja hata wakitokea benchi jambo ambalo litaifanya mechi ya leo kunoga.
Hawa hapa nyota wanaokipiga ndani ya Yanga na Simba ambao wana hatari wakitoka benchi kutokana na kuusoma mchezo:-
Papy Tshishimbi, kiungo wa Yanga, ana pasi moja ya bao ambayo aliitoa mbele ya Biashara United bao lake lilifungwa na Tariq Seif kwenye mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 alichukua nafasi ya Mrisho Ngassa dk ya 70.
Ditram Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi Alliance aliingia dakika ya 45 akichukua nafasi ya Tariq Seif.
Yikpe Gnamien, kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho aliingia dakika ya 56 akichukua nafasi ya David Molinga, alifunga bao la pili kwa pasi ya Bernard Morrison.
Kwa upande wa Simba, Super Sub wa muda wote ni Miraj Athuman ambaye alifanya maajabu yake kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania alipoingia dk ya 60 kuchukua nafasi ya Deo Kanda alifunga bao moja wakati Simba ikishinda mabao 3-1, mbele ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikishinda mabao 2-1 aliingia dk ya 62 akichukua nafasi ya Hassan Dilunga pia mbele ya Kagera Sugar wakati Simba ikishinda mabao 3-0 aliingia dk ya 61 akichukua nafasi ya Deo Kanda alisababisha penalti iliyofungwa na Meddie Kagere.
Ibrahim Ajibu, kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Taifa aliingia dk ya 45 akichukua nafasi ya Sharaf Shibob alifunga bao la ushindi dk ya 90 na kuipa pointi tatu timu yake.
Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Azam FC aliingia dk ya 63 akichukua nafasi ya Deo Kanda alifunga bao la ushindi wakati Simba ikishinda mabao 3-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment