March 8, 2020



2008/2009 mpaka 2019/20 Yanga na Simba zikiwa zimekutana uwanjani kwenye mechi 23 nyavuni yameokotwa mabao 51.

 Yanga imekuwa na ngekewa ya kufunga mabao mapema ndani ya dakika 15 za mwanzo wakiwa wamefunga mabao manne huku Simba ikiwa imefunga mabao matatu kwenye jumla ya mabao saba ya mapema ndani ya dakika 15 za mwanzo.

Bao la Emannuel Okwi lililofungwa dakika ya pili bado rekodi yake haijavunjwa huku Simba ikifunga mabao mawili ndani ya dakika 3 kwa misimu miwili tofauti na wachezaji wawili tofauti.

Leo kazi itakuwa kumtafuta atakayevunja rekodi zilizowekwa na wababe hao ambazo zilikuwa namna hii;- 2008/09, Oktoba 26,2008, Yanga 1-0 Simba, Ben Mwalala dk 15. 2012/2013, Mei 18,2014, Yanga 2-0 Simba, Didier Kavumbagu dk 5. 2012/13,Oktoba 20,2013, Yanga 3-3 Simba, Mrisho Ngassa dk 15. 2015/16, Oktoba Mosi,2016, Simba 1-1 Yanga, Simon Msuva dk 5.

Kwa upande wa Simba, 2009/2010, Aprili 18,2010, Simba4-3 Yanga, Uhuru Seleman dk 3. 2011/12, Mei 6,2012, Simba 5-0 Yanga, Emmanuel Okwi dk 2. 2012/13, Oktoba 3,2013, Simba 1-1 Yanga, Amri Kiemba dk 3.



2 COMMENTS:

  1. Nashukuru kwa kumbukumbu. Yanga mabao 4 ndani ya dakika 15 na Simba mabao 3 ndani ya dakika 15 za mwanzo.

    Lakini umesema mabao ya mapema zaidi ni ya simba.

    Nikitazama kichwa cha habari " Yanga kwa kucheka na nyavu mapema mbele ya simba balaa"
    Kwa uweledi wa mlinganisho hapo inagoma. Yaweke kwa ratio ama asilimia kwa kulinganisha hayo magoli kwa kutazama ya mapema zaidi.

    ReplyDelete
  2. Duh yani saleh jembe nimeamin kweli ni shida mbona kichwa cha habari na yaliyomo ndani ni tofauti kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic