March 23, 2020


MTAMBO wa kutupia ndani ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa chanzo kikubwa cha yeye kufunga hat trick kwenye mechi zao ni kutokana na msukumo wa kutaka kufunga mabao mengi kwenye kila mechi.

Nyota huyo raia wa Rwanda amesema kuwa anapenda kutumia kila nafasi anayopata kufunga jambo linalomfanya aweze kufunga hat trick.

Msimu huu, Kagere amefunga hat trick moja mbele ya Singida United ambapo Simba ilishinda mabao 8-0 Uwanja wa Uhuru.


"Nikipata nafasi napenda kuitumia na kufunga kadri unavyofunga ndivyo unajiongezea nafasi ya kufunga zaidi ndio maana ninafunga kila ninapopata nafasi,".

Msimu uliopita ambapo alimaliza akiwa amefunga mabao 23 alifunga hat trick moja mbele ya Coastal Union wakati Simba ikishinda mabao 8-1 Uwanja wa Uhuru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic