March 23, 2020


TIMU ya Namungo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imeshinda idadi ya mechi 14 ambazo ni sawa na ilizoshinda Yanga msimu huu wa 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Yanga iliyo chini ya Luc Eymael imecheza mechi 27 na kushinda mechi 14 za ligi zinazoifanya iwe nafasi ya tatu kwenye msimamo na kibindoni ina pointi 51.

Timu hiyo imekuwa ikila sahani moja na Yanga ambapo kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.


Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo imecheza mechi 28 na kushinda mechi 14 ndani ya ligi zinazoifanya iwe na pointi 50 kibindoni .

Mechi iliyowakutanisha Machi 15, Uwanja wa Majaliwa timu hizi zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na yote yalifungwa kwa kichwa.

Yanga ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya nne kupitia kwa kichwa cha Tariq Seif kwa pasi ya Juma Abdul huku Namungo wakifunga dakika ya 62 kwa kichwa cha Bigirimana Blaise kwa pasi ya Luka Kikoti.

1 COMMENTS:

  1. Yani kufunga simba lile goli la kubahatisha basi leo ni mwezi mzima sifa ndio huyo tu? Anamagoli mangapi? Na akina kagere wanamagoli mangapi kweli hawa ni vyura kandambili GONGOWAZI na hayo magazeti yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic