March 22, 2020

ABDI Banda, nyota wa Tanzania anayekipinga ndani ya Klabu ya Highlands Parks ya nchini Afrika Kusini na inashiriki Ligi Kuu amesema kuwa aliogopa alipohisiwa kwamba amepata virusi vya Corona.

Nyota huyo alitengwa na timu yake na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wiki iliyopita kutokana na kuonekana akikohoa mara kwa mara jambo lililofanya madaktari wamtenge mbali na wenzake  na kumfanyia vipimo vya Corona.

Baada ya kufanyiwa vipimo vya Corona Banda aligundulika hana Virusi hivyo jambo ambalo limempa amani na anaendelea na shughuli zake kama kawaida kwa sasa.

"Nilipata hofu nilipohisiwa kwamba nina virusi vya Corona ukizingatia kwamba kulikuwa na maambukizi yameshaanza nchini Afrika Kusini, nashukuru Mungu nilipopimwa nilikuwa salama jambo ambalo linanifanya niendelee kuwa na amani.

"Kwa sasa tunachukua tahadhari ya kujikinga na virusi hivi vya Corona ambapo Ligi Kuu imesimamishwa pia hakuna kufanya mazoezi ya pamoja kila mmoja anafanya yeye mwenyewe peke yake ila tunaomba hili lipite maisha yaendelee kuwa vizuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic