March 29, 2020

MABEKI wawili ndani ya Simba inaelezwa kuwa nafasi yao ya kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2020/21 ni ndogo kutokana na kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza hivyo panga linawahusu.

Nyota hao ni Paul Bukaba anayekipinga ndani ya Namungo kwa mkopo inaelezwa hajaweza kureea kwenye ubora wake pamoja na Yusuph Mlipili ambaye yupo Simba kwa sasa.

Mlipili, Simba ikiwa imecheza mechi 28 za Ligi Kuu Bara hajapata nafasi ya kuanza kwenye mechi hizo huku Bukaba akizidi kujiimarisha ndani ya Namungo.

Habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa ni kwamba Simba inataka kuboresha kikosi chake kwa kuleta nyota wengine ambao watachukua nafasi za wachezaji hao.

"Ili Simba ilete wachezaji ni lazima wengine waondoke kwani wapo wengi na nafasi zao pia zimekuwa finyu hivyo ni wakati wa kuangalia namna gani panga litawapitia," ilieleza taarifa hiyo.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck hivi karibuni alisema kuwa kwa wachezaji alionao kwenye kikosi chake wale ambao hawaanzi kikosi cha kwanza ni kutokana na juhudi wanazoonyesha kwenye mazoezi.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 kwenye msimamo.

10 COMMENTS:

  1. Fukuza tu sajirini wachezaji wazuri na wenye uwezo sio ilimradi tu wachezaji hii klabu kubwa afrika sio sawa na hao gongo wazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe hata kadi ya uanachama huna,wacha gongo wazi yetu

      Delete
  2. Huwezi kubaki na Wawa (34yrs) halafu ukamwondoa Mlipili mwenye umri mdogo.Practically simba haina uwezo wa kushindana na timu kubwa kusajili mchezaji mwenye uwezo mkubwa ambaye kimsingi huwezi kumpata kwa chini 500Mil....dirisha kubwa lililopita kulithibitisha hilo na klabu kubwa kama TP Mazembe wame-opt kutengeneza timu kwa kusajili vijana wenye uwezo. Shida yetu simba tunataka shortcut....Wawa+Nyoni sio beki za CL tukienda nao hawa zile tano tano zitajirudia.....halikadhalika Boco na Kagere umri imewatupa mkono.Ebu viongozi wetu tumieni ifanyike scouting nzuri ndani ya africa tupate wachezaji wazuri na vijana wenye uzoefu kidogo wa mechi kubwa za kimataifa halafu wasaidiwe na wakongwe wachache.....tujipe muda na tuambiane ukweli kuwa subira na muda vinahitajika kuelekea mafanikio ya kweli.Kwa maoni yangu ni mara mia umeamua kubaki na Mlipili kuliko Wawa mzee.Mlipili ni bora anachohitaji na game time......Lechantre angekuwepo huyu dogo angekuwa mbali mno. Hawa makocha wa sasa kuanzia Ausems wanakosa na wazoefu kumlinda ajira zao lkn hawasaidii simba kuimarika....hivyo viongozi ni lazima walilazimishe benchi la ufundi kuwasaidia vijana kukua na wawawekee makocha malengo ambayo ni realistic

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea point sana mzee hongera hivyo ndivyo inatakiwa ili simba iendane na hadhi yake

      Delete
    2. Swadkta kwa hoja uliyotoa.Makocha hawa kama Aussems na sasa Sven wanafundisha kwa ajili ya kutengeneza CV zao.Lenchatre alikuwa ana maono kwa vijana na Mlipili nitamkumbuka ile mechi Simba vs Al Masri lkn tokea amekuja na kuondoka Aussems na sasa Sven naona kama wamembania huyu kijana na soka yake ya 'Orlando'.Sven ndio simuelewi-elewi kwa kutowapa mechi kina Rashid Juma, Mpilipili, Ndemla, Ali Salim na Ajib kwa nadra sana.Inakatisha tamaa na kuna faida gani kumsajiri mchezaji na asitumikie timu msimu wote wa ligi?

      Delete
    3. Nan kakudanganya kuwa mlipili ana umri mdogo? fatilia historia ya mlipili utaona udogo na ukubwa wake

      Delete
  3. Tatizo la timu zetu za tz tunapenda kua na wachezaji ambao wameshatengenezwa...
    Hatutaki kua na wachezaji ambao tumewatengeneza wenyewe.
    Hata tukiwa nao tulio watengeneza tunashindwa kuvilinda viwango vyao....
    Mm naona kam mlipili angekua anapewa nafasi ni mchezaj mzuri kulko hata Santos...nakutakia safar njema mlipili uko uendako ila Asante kwa msaada wko ktk Tim yetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Enter your reply...ni maoni tu lakini siyo lazima yawe kweli au yakubaliwe

      Delete
  4. Ni mtazamo tu, madogo hawa nao ni shida wakipewa mechi wanadelay sana, mbona Luis kaja na anaonyesha yake, hii sio club ya majaribio waende simba B hapa ni kazi kazi

    ReplyDelete
  5. Kumuacha Mlipili bola uwaache wachezaji wote wanao cheza sehamu mabeki wa kati tuna mhitaji Mlipili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic