IMEELEZWA kuwa Uongozi wa Yanga unapiga hesabu za kushusha mashine nne za kazi ndani ya kikosi hicho ili kuongeza nguvu za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Wachezaji wanaopewa nafasi ya kuibukia ndani ya Yanga ni pamoja na mshambuliaji wa Namungo ambaye ni nahodha pia, Reliants Lusajo mwenye mabao 11 pamoja na Sixtus Sabilo huku wengine wawili ikiilezwa kuwa ni wachezaji wa kigeni.
Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hawana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuachwa kwa idadi ya pointi 20 na Simba.
Yanga ina pointi 51 ikiwa nafasi ya tatu huku Simba ikiwa na pointi 71 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo kwa sasa imesimama kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Hatutaweza kusema kwa sasa tunaweza kutwaa ubingwa wa ligi kutokana na kuachwa kwa pointi nyingi na wapinzani wetu hivyo ni lazima tujipange kwa ajili ya wakati ujao na kuwa na wachezaji makini ambao watatuupa matokeo chanya," amesema.
Kocha akituvunja moyo msimu huu basi hali kama hiyo itakuwepo mapema msimu ujao
ReplyDelete