MSHAMBULIAJI wa timu ya Ndanda SC ya Mtwara, Vitalis Mayanga amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2019/2020.
Nyota huyo anayekipiga ndani ya Ndanda FC ya Mtwara amewashinda Reliants Lusajo na Blaize Bigirimana wote wa Namungo alioingia nao fainali.
Mayanga alirejea ndani ya kikosi chake cha zamani cha Ndanda akitokea KMC baada ya mambo kuwa magumu ndani ya kikosi cha KMC.
0 COMMENTS:
Post a Comment