March 10, 2020


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amewapoteza makocha wenzake wawili ndani ya Ligi Kuu Bara ndani ya mwezi Februari alioingia nao kwenye kuwania tuzo ya kocha bora.

Sven ameteuliwa na Kamati ya Tuzo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutwaa tuzo hiyo akiwapiga chini Hitimana Thiery wa Namungo FC na Abdul Mingange wa Ndanda FC. 

Hii inakuwa tuzo yake ya kwanza baada ya kujiunga na Simba akipokea mikoba ya kipenzi cha mashabiki Patrick Aussems 'Uchebe' ambaye alipigwa chini. 

Mwezi Januari alishindana na Arstica Cioaba aliambulia patupu na tuzo hiyo kusepa kuelekea Azam FC kwa Cioaba. 

Thiery wa Namungo ni miongoni mwa makocha wanaofanya vema kwa sasa akiwa na kikosi chake kilichopanda daraja msimu huu kipo nafasi ya nne kikiwa kimejikusanyia pointi 48 baada ya kucheza mechi 26.

Mingange wa Ndanda taratibu anakitoa kikosi chake kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja kikiwa nafasi ya 16 na pointi zake 27 kimecheza mechi 26.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic