KWENYE mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa King Power kati ya Leicester City dhidi ya Aston Villa usiku wa kuamkia leo mambo yamekuwa mazito kwa Villa ya Mbwana Samatta baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0.
Harvey Barnes alianza kuitungua Villa dk ya 40 Jamie Vardy alipachika bao la pili dakika ya 63 mkwaju wa penalti kabla ya kurejea tena kambani dakika ya 79 huku mkwaju wa mwisho ukipachikwa na Barnes tena dk ya 85.
Aston Villa haikuambulia bao kwenye mchezo huo ambao mabeki walionekana kupoteana mwanzo mwisho.
Matokeo hayo yanaifanya Villa kuwa nafasi ya 19 ikiwa imecheza mechi 28 kwenye msimamo ikiwa na pointi 25 na Leicester City kuwa nafasi ya tatu na pointi 53 ikiwa imecheza mechi 29.
0 COMMENTS:
Post a Comment