MIKEL Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakicheza kwenye kiwango anachokipenda.
Arteta amekuwa akiwatumia makinda kwenye mechi za hivi karibuni na wakati akishinda kwa mabao 2-0 mbele ya Portsmouth kwenye mchezo Kombe la FA England.
Mabao ya Arsenal iliyofanya mabadiliko ya wachezaji Tisa kwenye kikosi cha Kwanza yalipatikana kupitia kwa Eddie Nketiah na Sokratis Papastathopoulos.
Arteta amesema:-" Ilikuwa ni kama vile kucheza kamari, tulifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Kwanza lakini nashukuru Mungu kwa kuwa wengi wamekuwa wakionyesha kitu cha tofauti. 'Ni vema nikawapongeza wachezaji wangu kwa kuonyesha viwango vya juu katika mechi zetu wanastahili kufanya hivyo kwenye mechi zote na kufuzu hatua inayofuata,".
0 COMMENTS:
Post a Comment