March 20, 2020




NYOTA wa kigeni ndani ya kikosi cha Simba wameonekana na balaa kwenye kucheka na nyavu huku wakiwapoteza wazawa ndani ya kikosi hicho cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Simba ikiwa ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28 imefunga mabao 63 ambapo wazawa wamefunga mabao 22 na wageni wamefunga mabao 41 wakiwapoteza pia wafngaji wa Yanga ambao jumla wametupia mabao 31 kwenye mechi 27.

Kinara wa kutupia mabao kwa wageni ambaye pia anakimbiza kwenye ligi ni Meddie Kagere raia wa Rwanda mwenye mabao 19 akifuatiwa na Deo Kanda raia wa Congo mwenye mabao 7, Francis Kahata raia wa Kenya ametupia mabao manne huku Lusi Miqussone raia wa Msumbuji, Gerson Fraga raia wa Brazil  wakitupia mabao matatumatatu kila mmoja.

Sharaf Shiboub raia wa Sudan na Clatous Chama raia wa Zambia wakitupia mabao mawilimawili, Tairone Santos raia wa Brazil  ametupia bao moja.

Kwa upande wa Yanga mgeni anayekimbiza kwa kutupia ni David Molinga mwenye mabao nane akifuatiwa na Patrick Sibomana mwenye mabao matano huku Bernard Morrison akitupia mabao matatu, Haruna Niyonzima, Yikpe hawa wametupia bao mojamoja.

Kwa upande wa wazawa ndani ya Simba, Miraj Athuman ‘Sheva’ na Hassan Dilunga wanaongoza jahazi kwa kutupia mabao sita kila mmoja wakifuatiwa na nahodha John Bocco mwenye mabao manne, Jonas Mkude na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wametupia mabao mawilimawili huku Ibrahim Ajibu na Erasto Nyoni wakitupia bao mojamoja.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic