ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kuna ulazima wa wachezaji wake kuongeza kasi ya kupambana ili kupata matokeo chanya kwenye mechi zao.
Katwila amesema kuwa ligi imekuwa na ushindani mkubwa na kila mechi wanayocheza ni ngumu jambo linalohitaji umakini.
"Wapinzani wetu wanapambana kupata matokeo nasi ni lazima tupambane kupata ushindi kwani tukishindwa kupata matokeo hatutakuwa kwenye nafasi ambayo tunaifikiria," amesema.
Mtibwa Sugar mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United Uwanja wa Gairo, Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment