March 21, 2020


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa  muda wa mapumziko kwa sasa utawarejesha kwenye morali wachezaji wake.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda wa siku 30 na Serikali ya Tanzania ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 50.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa :"Kwa sasa wachezaji wangu watapata angalau muda wa kupumzika kwani walikuwa wakicheza chini ya kiwango ambacho walikuwa nacho awali.

"Tunatambua kwamba kwa sasa kuna maambukizi ya Virusi vya Corona ni lazima tuchukue tahadhari na kutumia mapumziko vema kwani hili ni janga la dunia nzima kiujumla," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic