NYOTA wa Azam FC, Andrew Simchimba amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi hicho na ataendelea kuonyesha juhudi ili kufikia malengo aliyojiwekea yeye pamoja na timu.
Nyota huyo amerejea nyumbani baada ya kutolewa kwa mkopo kuitumikia timu ya Coastal Union ya Tanga kwa sasa yupo ndani ya jeshi la Azam FC lililo chini ya Arstica Cioaba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Simchimba amesema :-"Maisha ya soka ni ushindani mkubwa na kwa sasa hapa nilipo ninafurahi kuona kwamba ninapata ushirikiano mkubwa na harakati zinakwenda mdogomdogo.
"Malengo yangu ni kuona yale niliyojiwekea pamoja na ya timu yanakamilika kwa umakini jambo litakalojenga heshima kwangu na timu kiujumla,".
Simchimba ameongezewa kandarasi yake na mabosi ndani ya Azam FC atadumu ndani ya klabu hiyo mpaka 2023.
0 COMMENTS:
Post a Comment