March 10, 2020


JAFFARY Mohamed, beki kiraka wa Yanga amesema kuwa hakuwa na presha alivyopangwa kucheza na Simba kutokana na kuamini uwezo wake na kuwajua wapinzani wake vizuri.

Mohamed alionyesha uwezo wa hali ya juu kwenye mechi ya dabi ambayo kwake ilikuwa ya kwanza akiwa na Yanga alishuhudia timu yake ikiitungua Simba bao 1-0 ambalo liliwafanya wasepe na pointi tatu mazima Uwanja wa Taifa, Machi 8.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mohamed amesema kuwa alitambua kwamba wapinzani wake ni bora jambo ambalo aliliweka akilini na kuwaheshimu huku akiingia uwanjani bila kubeba presha.

"Mchezo wa mpira inategemea namna utakavyowakuta wapinzani wako wao wakikaza nasi tunakaza, hivyo sikuwa na presha niliamini utakuwa mchezo mgumu ila nilipewa majukumu ya kufanya na nilitimiza.

"Kushinda kwetu naona imeturudishia furaha ambayo ilikuwa imepotea ila kwa sasa hesabu zetu ni kuona nini tutafanya kwenye mechi zetu nyingine," .

Yanga imecheza mechi 25 imejikusanyia pointi 50 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic