UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la mchezaji wao Papy Tshishimbi kusepa ndani ya timu hiyo muda utaongea na atafurahia maisha akiwa ndani ya Klabu ya Yanga.
Tshishimbi raia wa Congo ambaye ni nahodha wa Yanga amesema kuwa mkataba wake umebaki miezi minne na amepata ofa nyingi ndani ya Bongo na nje ya nchi huku habari zikieleza kuwa anaweza kuibukia ndani ya Klabu ya Simba.
"Nimesikiliza ofa nyingi na ni kitu ambacho siwezi kuficha unaweza ukasema labda Simba sijui, timu gani nyingine lakini nina ofa nyingi na mkataba wangu wa mwaka mmoja ndani ya Yanga umebakiza miezi minene bado sijasaini mwingine," amesema.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:-"Umahiri wako,utimilifu wa kazi yako na thamani yako ipo pale palepale Papy Tshishimbi ila muda utaongea na naamini utaendelea kufurahia maisha ukiwa Yanga,".
Riverse:......Bonny Ndanje (Marehemu), Athmani Iddi "Chuji" na Mbuyi Twite...haya yote ni majina yaliyofanya namba Sita ya Yanga iwe imara..lakni sasa kuna Feisal Salum anaemfanya Tshishimbi asogezwe eneo lingne la kazi uwanjani. Twende sasa kwenye uwandishi wa Habari kuongeza thamani ya mchezaji kwa kuandikwa sana. Lakni kwa kuwa hakuna habari nzuri kwenye vyombo vya habari lazima kutafutwe kitu muhimu kingine. Wapo wengi tu wanaomaliza mikatabata..we unahic kwanini Tshishimbi???
Kwa hakika time haipo upande wenu na kila kitu kitajifichua si mbali
ReplyDeleteRiverse:......Bonny Ndanje (Marehemu), Athmani Iddi "Chuji" na Mbuyi Twite...haya yote ni majina yaliyofanya namba Sita ya Yanga iwe imara..lakni sasa kuna Feisal Salum anaemfanya Tshishimbi asogezwe eneo lingne la kazi uwanjani. Twende sasa kwenye uwandishi wa Habari kuongeza thamani ya mchezaji kwa kuandikwa sana. Lakni kwa kuwa hakuna habari nzuri kwenye vyombo vya habari lazima kutafutwe kitu muhimu kingine. Wapo wengi tu wanaomaliza mikatabata..we unahic kwanini Tshishimbi???
Deletepoint kaka
Deletegood
ReplyDelete