March 27, 2020

WACHEZAJI wa Simba wamejikuta wakiingia ndani ya mtego wa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.

 Machi 17, mwaka huu, Serikali ilitangaza kusimamisha shughuli mbalimbali ikiwemo za michezo na Ligi Kuu Bara kusimamishwa kwa siku 30.

Baada ya kutokea hilo, viongozi wa klabu mbalimbali waliwapa mapumziko wachezaji wao huku makocha wakiacha program maalum kwa wachezaji ili ligi ikiendelea wawe fiti kwa mapambano.

Taarifa kutoka katika benchi la ufundi la Simba zinasema kuwa, lina wasiwasi kuna baadhi ya wachezaji wao hawafuati program za kocha, hivyo wamepanga kuwawekea mtego wakirudi kambini.

“Unajua kwanza kufanya mazoezi ni tabia ya mtu binafsi na ni ngumu kujua kama mchezaji anafanya mazoezi au hafanyi, ili kutambua hilo, wakirudi kambini tutawafanyia vipimo vya utimamu wa mwili tujue kama walikuwa wanafanya mazoezi kulingana na program au la,” alisema mtoa taarifa huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic