March 22, 2020

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa iwapo tamko la Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) litaamua kuwazuia wachezaji waliovuka mipaka ya Tanzania kutokucheza mechi za Ligi Kuu Bara kutawavurugia mipango yao kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuondoka.

Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF alisema kuwa hakuna mchezaji atakayepewa ruhusa ya kucheza iwapo alitoka nje ya nchi kwa kuvuka mipaka kwa muda huu ambao Ligi Kuu Bara imesimamishwa.

"Hakuna ambaye amepewa ruhusa ya kuondoka nje ya ya nchi kwani sio likizo bali ni sitisho kwa muda kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi ya Corona hivyo kwa mchezaji ambaye atatoka nje ya nchi hataruhusiwa kucheza mechi zote ambazo zitaendelea ili kujikinga zaidi," alisema Karia.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa iwapo tamko hilo litakuwa hivyo watapata athari kutokana na mchezaji wao Molinga (David) na Kocha Mkuu, Luc Eymael kuwa nje ya nchi.

"Tutaathirika kutokana na tamko hilo kwani Molinga na Kocha Mkuu hawapo nchini kwa sasa tuliwapa ruhusa hivyo tutakachokifanya ni kuwasiliana na TFF ili kujua namna gani tutaliweka sawa jambo hili ikishindikana basi hatutakuwa na na namna nyingine," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Hur ni kukurupuka. TFF walisema kwamba wachezaji wote watapimwa.Sasa tatizo lipo wapi?Assume kwamba mchezaji raia wa Tanzania amekwenda Kenya nae atazuiwa kurudi na kucheza??Waandishi wakemee na kukosoa tamko hilo ambalo linapingana na agizo la Rais Magufuli kwamba wageni wanaotoka Nchi zilizoathiriwa sana nä Corona watengwe kwa siku 14 tena kwa gharama zao.Utamhukumu vipi mchezaji au kocha aliyeondoka kabla agizo halijatolewa?Kukurupuka kutoa maagizo yasiyo na tija kunaonyesha tulivyo kosa umakini kwenye uongozi wa TFF.

    ReplyDelete
  2. Wachezaji wote wa kigeni wana familia zao na sio waajiriwa wa TFF.Anakurupuka kiongozi eti hawawezi kuruhusiwa kucheza wakirudi!!Ruhusa ametoa nani ya kusafiri??TFF au klabu zilizowaajiri?Je ingekuwa ligi haijasimama TFF ingetoa tamko hilo?TFF man kazi za maana zaidi katika kuendeleza soka nchini.Wacheni kukurupuka.

    ReplyDelete
  3. juu ya hayo yote kwanini Walingoja wachezaji wasafiri ili watowe amri hiyo badala ya kutoa pale tu ilipotoka amri ya kusitisha ligi?

    ReplyDelete
  4. Ndio zao kukurupuka. Unangoja wachezaji wasafiri halafu unatoa kibao.Sasa kuwapima kabla ya ligi kuanza tena inakuwa na faida gani??Rais Magufuli keshasema wageni waruhusiwe lakini walipie karantini ya siku 14 tena ni wale wanaotoka Nchi ziliathiriwa sana na Corona Virus sio kila wageni.

    ReplyDelete
  5. Huyu Karia na TFF hawajui uongozi. Wachezaji wanazo haki zao za msingi kama binadamu mwingine yeyote. Huwezi kumzuia kusafiri isipokuwa atafuata sheria za nchi na utaratibu wa Serikali uliowekwa. Hatuwezi kuweka wachezaji wawe na sheria yao ya kuingia na kutoka nchini na Serikali nayo iwe na zake, hapana. Wote watafuata sheria za nchi na miongozo inayotolewa na Serikali yenyewe. TFF acheni msituvuruge.

    ReplyDelete
  6. TFF MMEFELI KWENYE HILI MSIWE KAMA MAKABURU WALIVYOWAWEKEA SHERIA WAAFRIKA KULE KUSINI ZILIZOKOSA UTU.

    ReplyDelete
  7. Huu ni kama mtego uliofichwa uukanyage ukunase. Ilibidi baada ya kuzuwa mechi ijuilishwe mapema haruhusiwi mchezaji kuondoka na pindi akiondoka hatoruhusiwa kushiriki Katika klabu yake lakini hayo hayakutokea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic