March 16, 2020

UJUMBE huu kwa mashabiki wa Simba na Yanga kutoka kwa Saleh Jembe:- Hongera sana mashabiki wa Simba, kwani licha ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watani wenu Yanga lakini mmechangia kwa kiasi kikubwa kuandika rekodi ya kujaza watu wengi zaidi mwenye uwanja wa Taifa.




Mashabiki wa Simba ndio waliojitokeza kwa wingi zaidi katika mechi hiyo na hii rekodi inawahusu. Hongera pia mashabiki wa Yanga ambao kwa 30 hadi 38% pia mlijitokeza Taifa siku hiyo mkiwa wenyeji, lakini NISISITIZE, si sawa na haitakiwi watu kuendelea kuhujumu mapato kwa kuwa wanakuwa wanahujumu mapato ya hizi klabu lakini Serikali pia.

9 COMMENTS:

  1. VITENDO VYA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE MAPENZI NA SIMBA

    Mbona watu wa Simba wamekasirika sana mpaka viongozi wa serikali (Waziri Mkuu-Namungo fc & Mkuu wa Mkoa Dsm-Simba&KmC) ambao hawapaswi kuegemea upande wowote wanaipania Yanga (utafikiri Yanga ni timu kutokea Kenya) na wanaonyesha mapenzi yao dhahiri na kwa uwazi hili si jambo zuri na linaweza kuleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii iliyo na umoja uliojengwa na waasisi wa Taifa hili...(Mwl. Nyerere, na Sheikh Karume). Mambo ya Mpira yasitugawe katika umoja wetu na Viongozi waliopewa dhamana ya utawala kwa wananchi....dini zetu, mapenzi yetu kwa timu za mpira yasitugawe!

    sikatai kuhamasisha michezo katika jimbo lake la uchaguzi ila Waziri Mkuu anapotoa kauli yenye amri na maagizo yenye utashi binafsi kwa uongozi wa wilaya kumbuka timu pinzani na waamuzi hufikia kwenye mahoteli na guests zote hizo ziko wilayani kunaweza kukawa na shinikizo la hujuma kufanyika kwenye mchezo husika....hiyo ndiyo hoja yangu. Na pia pale Mkuu wa Mkoa anapoingilia katika kuitunza ahadi ya fedha timu moja iliyo katika Mkoa mmoja na timu pinzani, inaleta taswira ya upendeleo na inajenga imani ya chuki kwa timu nyingine....mapenzi binafsi ya viongozi wa serikali katika timu za mpira nasisitiza kwa mara nyingine yasitugawe na yasitutenganishe kwani huu umoja na mshikamano wa kitaifa na udugu ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu...mwalimu Nyerere na Sheikh Karume na muda mrefu.....(hata wao walikuwa na mapenzi ya timu za soka) lakini hawakuwahi kukandamiza timu nyingine!

    Ni maoni yangu
    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. Wache wapendao wapende kwani mapenzi yameumbwa moyoni kwani hata baba na mama wenye watoto Mara nyingi hutokea kidogo akamili kwa huyu kuliko huyukwani pendo ni kitu cha khiari sio cha kulazimishwa au kuelekezwa

    ReplyDelete
  3. Kwakuwa Yanga wamekanyagwa na KMC ndio kusema Makonda ameonesha kuikamia Yanga? Huo ni ujinga.Ligi kuu mara hii ina upinzani na ni dalili njema kwa soka letu. Namungo kutoka sare na Yanga halafu unalia kusema Waziri mkuu anaikamia Yanga huo ni ukichaa. Mashabiki wa yanga ni watu wa hovyo siku zote kwani timu yao ikishinda,kelele za kuwa timu yao ni kiboko huwaga mpaka zinakera lakini wakifungwa wameonewa? Mechi na Simba wamepata bao la uchawini mlichonga hadi kufuru. Singida aliepigwa nane na Simba kaenda kumpiga mbeya city utaona namna ligi ilivyokuwa haitabiriki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukosawa kabisa Mkuu niteam ya watu wanaolalamika Sana nani anawakamia walivyo ifunga Simba nani aliwakamia wacheze moira waache kulia lia

      Delete
    2. Unazi kwa Kiongozi mwenye dhamana ya kiserikali ulio waziwazi na mashinikizo lazima yakemewe kama tunataka kuendelea kisoka na ndio maana timu hazifiki mbali zinapoenda kwenye mashindano ya kimataifa

      Delete
  4. Wanajisahaulisha walivyo kuwa wanatufanyia! nabado ngoja msimu unaokuja mtakula jeuli yenu SIMBA BABA LAO

    ReplyDelete
  5. Msola na fredrck tumempa kazi maalumu ili mnyooke

    ReplyDelete
  6. Pambaneni mpate nafasi ya 4 ndio yenu gongowazi

    ReplyDelete
  7. Hata hiyo nafasi ya nne ni mashaka.kocha wao ameshajikatia tamaa na timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic