TARIQ Seif, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuibuka na ushindi mbele ya Namungo FC kutokana na kukosa umakini.
Yanga wakati ikikubali kutoshana nguvu na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa kwa kufungana bao 1-1 wao walianza kufunga bao dk ya sita kupitia kwa Seif kabla ya Namungo kuweka mzani sawa dk ya 62 kupitia kwa Bigirimana Blaise.
Nyota huyo amesema: "Tulitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo na kushindwa kuzitumia kutokana na kukosa umakini ndani ya uwanja, tutafanyia kazi mapungufu yetu,".
Mchezo uliopita Yanga ilipoteza pointi tatu mazima mbele ya KMC jana Machi 15 imegawana pointi mojamoja na Namungo FC kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Bao hilo la kichwa alilofunga Seif ni la tatu ndani ya ligi ambapo la kwanza aliwafunga Biashara United kwa pasi ya Papy Tshishimbi akafunga mbele ya Polisi Tanzania kwa pasi ya Bernard Morrison na jana alifunga kwa pasi ya Juma Abdul.
VITENDO VYA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE MAPENZI NA SIMBA
ReplyDeleteMbona watu wa Simba wamekasirika sana mpaka viongozi wa serikali (Waziri Mkuu-Namungo fc & Mkuu wa Mkoa Dsm-Simba&KmC) ambao hawapaswi kuegemea upande wowote wanaipania Yanga (utafikiri Yanga ni timu kutokea Kenya) na wanaonyesha mapenzi yao dhahiri na kwa uwazi hili si jambo zuri na linaweza kuleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii iliyo na umoja uliojengwa na waasisi wa Taifa hili...(Mwl. Nyerere, na Sheikh Karume). Mambo ya Mpira yasitugawe katika umoja wetu na Viongozi waliopewa dhamana ya utawala kwa wananchi....dini zetu, mapenzi yetu kwa timu za mpira yasitugawe!
sikatai kuhamasisha michezo katika jimbo lake la uchaguzi ila Waziri Mkuu anapotoa kauli yenye amri na maagizo yenye utashi binafsi kwa uongozi wa wilaya kumbuka timu pinzani na waamuzi hufikia kwenye mahoteli na guests zote hizo ziko wilayani kunaweza kukawa na shinikizo la hujuma kufanyika kwenye mchezo husika....hiyo ndiyo hoja yangu. Na pia pale Mkuu wa Mkoa anapoingilia katika kuitunza ahadi ya fedha timu moja iliyo katika Mkoa mmoja na timu pinzani, inaleta taswira ya upendeleo na inajenga imani ya chuki kwa timu nyingine....mapenzi binafsi ya viongozi wa serikali katika timu za mpira nasisitiza kwa mara nyingine yasitugawe na yasitutenganishe kwani huu umoja na mshikamano wa kitaifa na udugu ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu...mwalimu Nyerere na Sheikh Karume na muda mrefu.....(hata wao walikuwa na mapenzi ya timu za soka) lakini hawakuwahi kukandamiza timu nyingine!
Ni maoni yangu
Ahsanteni
Mkuki kwa nguruwe, kwanini Hukulalamikia haya pindi mh Mwigulu alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alipomsainisha Feitoto mara 2 ilimradi tu atue Yanga? Pia Inakuuma nini KMC Kupewa m20 ilhali Yanga mlipewa uwanjA bure Kigamboni na huyuhuyu mkuu wa mkoa? Huu mchezo hauhitaji hasira tulieni data iwaingie
Deletendugu jiongeze kidogo kiuweledi unapotoa hoja....hoja yako ni dhaifu mno..Kumsajili mchezaji na kutoa kiwanja ni tofauti na kuuingilia mchezo na kutoa maagizo kwa vyombo vinavyousimamia mchezo wa soka na kushinikiza haki isitendeke
DeleteUmesahau maagizo ya Mkuu wa Mkoa Kagera wakati Simba ilipokwenda kucheza na Kagera Sugar? Ni Haji Manara pekee alimjibu bila woga huku wengine wakishangila, msumeno umegeuka upande mwingine mnapiga kelele.
Deletemkuu wa mkoa wa kagera alikua anataka watu washangilie timu ya mkoa wao
Deletelakini makonda amelala upande mmoja sababu Yanga na KMC pamoja na simba wapo mkoa wake na kama mkuu wa mkoa timu zote ziwe muhimu kwake asilete ubaguzi kama kiongozi wa mkoa wa Dar
Hameishi sababu kwasababu mnajinasibu sio wa kufungwa. Basi jipeni tamaa Kwa kusema mtashinda mechi zote zilizobaki na huku Mnyama atashindwa mechi zake zote zilizobakia
ReplyDeletekiwango yanga ya zorota !
ReplyDeletePamoja na hili pia kubali kuwa kuna ushahidi 100% wa hujuma na uonevu dhidi yao
DeleteMngepitia Ngende mngeshinda. Je millioni 200 zimetoka? Kama zimetoka bado wachezaji wanzikumbuka badala ya kuzitafuta nyingine
DeleteKubali hoja ya msingi kuwa mpira wa Tanzania umeingiliwa na wanasiasa
Delete