March 16, 2020

14 COMMENTS:

  1. VITENDO VYA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE MAPENZI NA SIMBA

    Mbona watu wa Simba wamekasirika sana mpaka viongozi wa serikali (Waziri Mkuu-Namungo fc & Mkuu wa Mkoa Dsm-Simba&KmC) ambao hawapaswi kuegemea upande wowote wanaipania Yanga (utafikiri Yanga ni timu kutokea Kenya) na wanaonyesha mapenzi yao dhahiri na kwa uwazi hili si jambo zuri na linaweza kuleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii iliyo na umoja uliojengwa na waasisi wa Taifa hili...(Mwl. Nyerere, na Sheikh Karume). Mambo ya Mpira yasitugawe katika umoja wetu na Viongozi waliopewa dhamana ya utawala kwa wananchi....dini zetu, mapenzi yetu kwa timu za mpira yasitugawe!

    sikatai kuhamasisha michezo katika jimbo lake la uchaguzi ila Waziri Mkuu anapotoa kauli yenye amri na maagizo yenye utashi binafsi kwa uongozi wa wilaya kumbuka timu pinzani na waamuzi hufikia kwenye mahoteli na guests zote hizo ziko wilayani kunaweza kukawa na shinikizo la hujuma kufanyika kwenye mchezo husika....hiyo ndiyo hoja yangu. Na pia pale Mkuu wa Mkoa anapoingilia katika kuitunza ahadi ya fedha timu moja iliyo katika Mkoa mmoja na timu pinzani, inaleta taswira ya upendeleo na inajenga imani ya chuki kwa timu nyingine....mapenzi binafsi ya viongozi wa serikali katika timu za mpira nasisitiza kwa mara nyingine yasitugawe na yasitutenganishe kwani huu umoja na mshikamano wa kitaifa na udugu ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu...mwalimu Nyerere na Sheikh Karume na muda mrefu.....(hata wao walikuwa na mapenzi ya timu za soka) lakini hawakuwahi kukandamiza timu nyingine!

    Ni maoni yangu
    Ahsanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hoja yako haina mashiko. Mpira unachezwa uwanjani. Kila timu inapambana kivyake kupata matokeo. Viongozi wa Serikali nao wana mapenzi yao kwa timu fulani, na huwezi kuwazuia. Tulikuwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye alionesha waziwazi unazi wake kwa Yanga. Nini kiliharibika? Makonda ni mlezi wa KMC ambayo ipo chini ya moja ya Manispaa za mkoa wake. Sioni ubaya yeye kuipa motisha KMC. Hali kadhalika, Waziri Mkuu inafahamika kwamba ni mlezi wa Namungo, kama alivyokuwa wakati ule Mwigulu (akiwa mlezi wa Singida Utd lakini pia akiwa mnazi wa Yanga. Ingawa tunajua Mwigulu alikuwa pia anaifanyia hujuma Simba. Acheni kutafuta visingizio, chezeni mpira. Ingekuwa hao wote unaowataja wanaihujumu Yanga, hivi kweli mngeweza kuifunga Simba?

      Delete
    2. Soma vizuri hoja ya msingi sikatai mtu au kiongozi wa serikali kuwa mnazi wa klabu ninachokipinga ni kutumia dhamana ya uongozi kuingilia Uamuzi wa mchezo na kushinikiza hujuma kwa timu fulani....hao unaowataja hawakuwahi kufanya hivyo isipokuwa tunaliona hili kipindi hiki..

      Delete
  2. Acha unazi, Mwigulu hakuwa kiongozi wa Serikali na alionesha mapenzi kwa Yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma vizuri hoja ya msingi sikatai mtu au kiongozi wa serikali kuwa mnazi wa klabu ninachokipinga ni kutumia dhamana ya uongozi kuingilia Uamuzi wa mchezo na kushinikiza hujuma kwa timu fulani....hao unaowataja hawakuwahi kufanya hivyo isipokuwa tunaliona hili kipindi hiki..

      Delete
  3. Hao viongozi unaosema wanawahujumu ndio wamewapa uwanja wa bure rudisheni Basi huo uwanja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kutoa uwanja ni tofauti na kushinikiza na kuchochea hujuma kupitia mlango wa nyuma

      Delete
  4. Ajaribu kukumbuka juwa hata jerry muro pia ni kiongozi wa serikali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jerry muro hakuwahi kutunza timu zawadi baada ya kumfunga Simba....hii ndiyo tofauti

      Delete
  5. mwigulu anaipenda Yanga na kaisaidia lakini makonda anaipenda simba na hapo hapo anatoa dau kushawishi timu nyingine kuifunga yanga na huo ndio utofauti kati ya mwigulu na makonda na kama mwelevu utaelewa

    ReplyDelete
  6. Mpira ni uwezo, simba iliahidiwa 300ml lakini ilishindwa kwa yanga iliyoahidiwa 200ml. Kama ahadi ya fedha ndyo kila kitu basi simba angeshinda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio uliewaahidi simba kuwapa 300milions?acha ujinga na unazi kijana,gazeti lako liliandika wapi kwamba simba imeahidiwa 300mil?kurasa zote zilikua zinaeleza habari za yanga tu.usiwe mnafiki muangalie.

      Delete
  7. Hilo gazeti badala ya kuandika matokeo ya namungo na yanga linaandika umbeya mwingine yanga mtateseka Sana mwaka huu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kwasababu bila ya makandokando Yanga haifungwi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic